Miradi bubu Musoma inaigharimu Manispaa.
Ukifika makao makuu ya mkoa wa mara nje ya ofisi yao kuu utakuta bango kubwaa limeandikwa maneno mengiii lakini linalovutia zaidi ya yote linasema tumedhamilia kulinda rasilimali za mkoa wa Musoma.
Mbele kidogo kuna mradi ulioandikwa umezinduliwa mwaka 2009 na Mh. Waziri wa wakati huo serina kombani akiwa waziri wa tamisemi, ambao upo chini ya manispaa, hapo ndipo unaanza kujiuliza ile kauli mbiu ya lile bango ni ya kweli au geresha?.
Kwa mara ya kwanza mradi huu ulizinduliwa wakati wa mbio za mwenge na kuitwa bustani ya mwalimu nyerere. Lakini hali ya hilo eneo inaonyesha haijawahi kutumiwa tangu huo ukumbi uliogharimu mamilioni ya shilingi kutokana na kodi za wananchi ulipozinduliwa.
Leo hii Mh. Kombani ni waziri wa katiba na sheria alichokizindua manispaa ya Musoma kinabaki kuwa ni aibu kwa serikali ya mkoa na nchi kwa ujumla. Cjui lengo la bustani ile lilikuwa ni kwa ajiri ya nani na kwa manufaa ya nani.
Kama walikusudia kujenga ukumbi wa mikutano mbona hawafanyii pale badala yake wanakodi kumbi za hotel za kifahari? Na kama walitenga eneo la kupumzikia wakati wa lunch mbona hajawahi kuonekana ata mkuu wa wilaya akipunga upepo pale? Huu ni uhujumu uchumi na lile bango walitoe waweke lingine.
Kwa sasa Ukumbi ndani yamegeuka kuwa makazi ya popo, kweli!!! Manispaa ijipambanue kwa hilo vinginevyo raisi akimaliza mgogoro wa madactari ajiandae migogoro mingine kwa kuwa hawa wakuu wa mikoa na wilaya ni mizigo tu. Na hakuna wanachokifanya zaidi ya kukinga mishahara.
Maryogo njoo ukague makazi yako uliyotumia mamilioni kujenga.
Ukifika manispaa ya Musoma mjini kuna eneo maarufu sana linaitwa kwa Maryogo. Simulizi za watu wa huku zinaeleza kuwa huyu mtu alikuwa ni barozi wa Tanzania nchi Italy miaka ya themanini.
Huyu jamaa inasemekana alijengewa nyumba na wafungwa wa magereza ya Musoma kwa niaba ya serikali. Mara ya kwanza aliibomoa kwa madai ilikosewa, mala ya pili akaibomoa tena. Mwalimu nyerere aliingilia kati na kumuuliza hivi Maryogo hii fedha unayoitupa hapo umeipata wapi?
Nyumba ikajengwa kwa mala ya tatu ndio gofu lililopo mpaka leo mwaloni mwa ziwa Victoria. Inasemekana aliwahi kuishi na mke wake mzungu kwa kipindi furani lakini tangu alipotokomea mpaka leo hakuna mtu.
Ni nyumba ya kifahari sana, lakini sasa hivi ata nyasi za kifahari alizopanda hazipo tena pamegeuka makazi ya BUNDI na wanyama poli kama pimbi na majoka. Kama lengo lake lilikuwa ni kufuga hao wanyama basi aje avune tayari wamekuwa.
Watanzania wa namna hii wanatakiwa wachunguzwe na mali zao kutaifishwa ikiwa itagundulika walihujumu uchumi, kwa kuwa walitumia rasilimali za umma na mabilioni ya shiringi kujitajirisha na kutelekeza mali na maeneo ya kufuru huku mikoani.
![]() |
geti la kuingilia kwenye mji wa maryogo alioterekeza |
![]() |
makazi ya kifahari yaliyoterekezwa na maryogo |
No comments:
Post a Comment