Friday, April 17, 2015

Undishi wahisia uishie kwa huyu jamaa JK.

nikizitazama sura za wagombea waliotangaza na wanaotajwa kugombea uraisi kwa vyama vyote... sioni sura ya subira itakayosemwa kama JK ikavumilia na kuwaacha wanahabari wafanye kazi yao japo kwa uchache

nasema tena sura zote hazina subira wala uvumilivu wa kukosolewa nathubutu kusema zote ni sura za kigaidi.

wanahabari mjiandae kufungwa na kupewa maonyo makali katika hotuba zao za kila mwisho wa mwezi..

 sishawishiki kuwa zikipewa madaraka labda zitabadilika.

Thursday, January 8, 2015

Pamoja Tuwale

2015 kwangu utakuwa wa kusaidia wasiojiweza hasa watoto. wewe je?
 wangapi utakuwa mwaka wa kupombeka?
wangapi utakuwa mwaka wa kuoana ndoa zetu zile?
wangapi utakuwa mwaka wa kufanya uwekezaji?
wangapi utakuwa mwaka wa kusamehe?
wangapi utakuwa mwaka wa kurudi darasani?
wangapi wanampango wa kuongeza idadi ya maadui?

mwisho wa yote...... wote kaburi halijatupa tarehe ya kuliiingia.